• HABARI MPYA

    Monday, May 04, 2026

    MBEYA CITY YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-1 UWANJA WA SOKOINE


    TIMU ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya ndugu zao, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanznaia Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Mbeya City yamefungwa na mshambuliaji Eliud Ambokile dakika ya 19 na beki Marco Mhilu aliyejifunga dakika ya 57, wakati bao pekee la Tanzania Prisons waliokuwa wenyeji wa mchezo limefungwa na winga Emmanuel Martin dakika ya 33.
    Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya 13, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 14 nafasi ya 15 baada ya timu zote kucheza mechi 21 kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-1 UWANJA WA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top