MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo, kiungo wa Kimataifa wa Uganda, Allan Okello ‘Star Boy’ dakika ya 65 na kwa ushindi huo Yanga wanafikisha pointi 51 katika mchezo wa 21 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 43 za mechi 21 pia na Simba SC pointi 43 za mechi 20.
Mambo yanazidi kuwa magumu kwa KMC ikiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi zake tisa baada ya kuch3za mechi 21.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment