• HABARI MPYA

    Sunday, May 03, 2026

    YANGA SC YATOKA NYUMA MABAO MAWILI NA KUTOA SARE 2-2 NA SIMBA MBWENI


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wametoa sare ya kufungana mabao 2-2 na watani wao, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Simba SC inayofundishwa na Kocha raia wa Afrika Kusini, Steven ‘Steve’ Robert Barker iliuanza vyema mchezo huo na kufanikiwa kupata mabao mawili ndani ya dakika 10 za mwanzo, winga wa kushoto Msenegal, Libasse Gueye dakika ya tatu na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 10.
    Hata hivyo, Yanga SC walio chini ya Kocha Mreno, Pedro Valdemar Soares Gonçalves wakasawazisha mabao hayo kupitia kwa mshambuliaji wake Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya 17 na beki mzawa, Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 50.
    Mchezo huo ulichezeshwa vyema na marefa kutoka Morocco, Hamza El Fareq aliyesaidiwa na Lahsen Agaou na Hamza Massiri pembezoni mwa Uwanja na Mustapha Kechaf mezani chini ya usimamizi wa mzawa, Soud Abdi wa Arusha.
    Kwa matokeo hayo, Yanga SC mabingwa mara nne mfululizo wa Ligi Kuu wanatimiza pointi 48 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya Simba SC baada ya timu zote kucheza mechi 20.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YATOKA NYUMA MABAO MAWILI NA KUTOA SARE 2-2 NA SIMBA MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top