• HABARI MPYA

    Friday, May 01, 2026

    DODOMA JIJI FC YAAMBULIA SULUHU KWA NAMUNGO FC 0-0 SINGIDA


    WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Airtel Mwigulu mjini Singida.
    Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 25 na inabaki nafasi ya nane ikiendelea kuizidi pointi mbili Namungo FC inayosaliia pia nafasi ya tisa katika ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 20.  
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI FC YAAMBULIA SULUHU KWA NAMUNGO FC 0-0 SINGIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top