WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Kwa matokeo matokeo hayo katika mchezo wa 22 kwa timu zote, Mashujaa FC inafikisha pointi 26 ingawa inabaki nafasi ta tisa na Namungo FC inafikisha pointi 24 katika nafasi ya 10 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment