• HABARI MPYA

    Tuesday, May 05, 2026

    NDUWUMWE AFUNGA MAWILI SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA PAMBA JIJI 3-1


    TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Airtel Mwigulu mjini Singida.
    Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na winga wa kulia wa Kimataifa wa Burundi, Mossi Nduwumwe mawili, dakika ya 21 na 53 na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malanga Horso Mwaku dakika ya 70, wakati bao pekee la Pamba Jiji FC limefungwa na mshambuliaji mzawa, Henry Msabila Lutonja dakika ya 90.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 21 na kupanda kwa nafasi tatu hadi ya nne, ikiishushia Pamba Jiji FC nafasi ya saba ikibaki na pointi zake 29 za mechi 21 pia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDUWUMWE AFUNGA MAWILI SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA PAMBA JIJI 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top