TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wapi mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah mawili, dakika ya nane na 58 na mshambuliaji Mkongo, Jephte Kitambala Bola dakika ya 20.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 40, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 23 nafasi ya 10 kwenye ligi ya timu 16, baada ya timu zote kucheza mechi 20.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment