TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Zambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 54 na kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 46 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tano na vinara na mabingwa watetezi, watani wao, Yanga SC baada ya timu hizo zote kucheza mechi 21.
Kwa upande wao JKT Tanzania baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 32 katika nafasi ya tano wakizidiwa tu wastani wa mabao na Singida Black Stars baada ya timu hizo pia kucheza mechi 21.



.png)
0 comments:
Post a Comment