• HABARI MPYA

    Monday, May 04, 2026

    MASHUJAA YAICHAPA TRA UNITED YA CHOBWEDO 1-0 KIGOMA


    TIMU ya Mashujaa United imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Bao pekee la Mashujaa FC limefungwa na mshambuliaji, Ismail Mohamed Mgunda dakika ya 37 na kwa ushindi huo timu hiyo ya Kocha Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya tisa, wakati TRA United inabaki na pointi zake 30 nafasi ya tano baada ya timu hizo zote kucheza mechi 21 kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHUJAA YAICHAPA TRA UNITED YA CHOBWEDO 1-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top