• HABARI MPYA

    Saturday, May 02, 2026

    COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 MKWAKWANI


    TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Mabao ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid Maabad dakika ya tatu kwa penalti na kiungo Bakari Suleiman Msimu dakika ya 16, wakati bao pekee la Singida Black Stars limefungwa na kiungo Mghana, Emmanuel Kwame Keyekeh dakika ya 50 kwa penalti pia.
    Kwa ushindi huo katika Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16, Coastal Union inafikisha pointi 22 na kusogea nafasi ya 11, wakati Singida Black Stars inabaki pointi zake 29 nafasi ya saba baada ya timu zote kucheza mechi 20. 
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top