TIMU ya TRA United imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mabao ya TRA United yamefungwa na kiungo Ally Hamisi Ng'anzi dakika ya 19, mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ami Buetusia Mapaka, mawili dakika ya 41 na 43 na winga Ramadhani Salum Ramadhani ‘Chobwedo’ dakika ya 63 kufuatia Azam FC kutangulia na bao la mshambuliaji wake, Mkongo (DRC), Jepthe Kitambala Bola.
Kwa ushindi huo, TRA United inafikisha pointi 33 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nne, ikizidiwa pointi 10 sasa na Azam FC baada ya timu zote kucheza mechi 22 kwenye Ligi Kuu inayoshirikisha timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment