• HABARI MPYA

    Wednesday, May 06, 2026

    DODOMA JIJI YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0 CHAMAZI MWISHO


    TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Bao pekee la Dodoma Jiji FC limefungwa na mshambuliaji William Edgar dakika ya 44 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 28, ingawa inabaki nafasi ya nane, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 23 za mechi 21 nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0 CHAMAZI MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top