![]() |
Taifa Queens |
TIMU ya Taifa ya netiboli ya Tanzania, Taifa Queens inashuka tena dimbani leo kumenyana na Zimbabwe, baada ya jana kuifunga Zambia,
Taifa Queens jana ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 37-33 dhidi
ya Zambia katika mchezo wa mashindano ya Afrika yanayoendelea kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Taifa Queens hadi robo ya kwanza
inamalizika ilikuwa imetanguliwa na Zambia kwa bao 8-6 na kuwatia presha
mashabiki na viongozi wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), waliofika
kuishangilia timu hiyo.
Baada ya kufungwa juzi na Malawi kwa
tofauti ya mabao machache, Taifa Queens ilihitaji
ushindi ili kurejesha matumaini ya kufanya
vizuri katika mashindano hayo.
Wachezaji wa Taifa Queens pamoja na kupata
nafasi nzuri lakini wafungaji wao hawakuwa makini na kusababisha kupoteza
nafasi nyingi za kufunga kwa sababu ya kukosa umakini golini.
Hata hivyo, timu hiyo ilibadilika kidogo na
katika robo ya pili ilicharuka na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 20-16 na
angalau kupunguza presha kwa mashabiki waliofika kuishangilia timu hiyo.
Katika robo ya tatu, wenyeji waliibuka na
ushindi wa bao 28-26 kabla ya kugangamala katika robo ya nne na ya mwisho na
kufanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 37-33.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mary Protas
akizungumza baada ya mchezo huo alisema kuwa, ulikuwa mgumu lakini wamefurahi
kulipa kisasi baada ya Zambia kuifunga Tanzania katika Michezo ya All Africa
Games iliyofanyika Maputo, Msumbiji.
Alisema wachezaji wake walicheza wakiwa na
mchecheto hasa baada ya kujua uzuri wa timu
hiyo na umuhimu wa kuibuka na ushindi dhidi
ya Wazambia, lakini watarekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo.
Taifa Queens ambayo leo itakuwa na kibarua
cha kucheza na Zimbabwe katika mfululizo wa mashindano hayo, ina pointi nne
baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Lesotho siku ya
ufunguzi na jana kuifunga Zambia. Taifa Queens walifungwa na Malawi.
0 comments:
Post a Comment