Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
CHELSEA, REAL MADRID ZAGOMBEA BEKI LA AJAX
KLABU za Manchester United, Manchester City na Chelsea zinamgombea mchezaji wa Fulham, Moussa Dembele. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa ubelgiji anamaliza mkataba wake Craven Cottage mwaka 2013, na pia anawaniwa na Arsenal, Liverpool na Tottenham.
Habari kamili: Metro
KLABU ya Tottenham inamtaka Ben Foster kurithi mikoba ya kipa wao, Brad Friedel mwenye umri wa miaka 40.
Habari kamili: Daily Mirror
KLABU ya Chelsea itaingia kwenye vita na Real Madrid na Roma kumgombea mchezaji Gregory Van Der Wiel. Beki huyo wa kulia wa Ajax mazungumzo yake na Valencia yamevunjika.
Habari kamili: talkSPORT
KLABU ya Manchester City imefanya mawasiliano kwa mara ya kwanza na Napoli juu ya mpango wa kumnunua Edinson Cavani, taarifa kutoka Italia zimesema.
Habari kamili: talkSPORT
KLABU ya Chelsea inatumai kuipiga bao Liverpool katika kuwania saini ya kinda la Partizan Belgrade la Seria, kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 18, Lazar Markovic, ambaye amependekezwa na Avram Grant.
Habari kamili: Daily Mail
KLABU ya Arsenal inaweza kujiunga kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa Borussia Dortmund, Shinji Kagawa. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Japan anataka kuiacha klabu hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia klabu kadhaa, zaidi ni Manchester United.
Habari kamili: caughtoffside.com
DALGLISH ANABAKI LIVERPOOL
KLABU ya Liverpool iko tayari kuendelea na kocha Kenny Dalglish, lakini atapewa fedha kidogo tu za kufanyia usajili wa wachezaji wapya.
Habari kamili: Daily Mirror
KOCHA Mark Hughes ametenga bonasi ya pauni Milioni 1 kwa wachezaji wake QPR, iwapo wataiwezesha timu hiyo kubaki Ligi Kuu wakicheza mechi ya mwisho na Manchester City Jumapili.
Wakati huo huo, beki wa Hoops, Nedum Onuoha amesema atakuwa na siku nzuri maishani mwake katika kucheza England, ikiwa Rangers itabaki Ligi Kuu Jumapili kwa kuifunga klabu yake ya zamani, Manchester City.
Habari kamili: Evening Standard
VAN PERSIE HANG'OKI EMIRATES
KLABU ya Arsenal inajiamini kwamba Robin van Persie atasaini mkataba mpya, licha ya kutakiwa na Juventus na Manchester City.
Habari kamili: Metro
0 comments:
Post a Comment