Lionel Messi
| Drenthe |
KLABU ya Barcelona imemtetea Lionel Messi dhidi
ya tuhuma za ubaguzi alizotupiwa na Royston Drenthe.
Mholanzi Drenthe, ambaye kwa sasa anachezea Everton kwa
mkopo, akitokea Real Madrid, alidai Messi alimuita "negro" mara
kadhaa wakati akicheza Hispania.
Barcelona imeyapuuza madai hayo na kusema Messi
hana tabia hiyo.
"Mchezaji huyo wakati wote amekuwa akionyesha
heshima kwa kiwango kinachotakiwa na uanamichezo kwa wapinzani wake," alisema
Msemaji wa Barca.
Drenthe mwenye umri wa miaka 25, akiwa
katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake Real Madrid, msimu huu amecheza kwa
mkopo Goodison Park, lakini hivi karibuni alienguliwa kwenye kikosi cha David
Moyes kwa utovu wa nidhamu.
Alijiunga na Real akitokea Feyenoord mwaka
2007 na msimu uliopita alichezea kwa mkopo Hercules ya Hispania.
Pamoja na kumuita negro mara kadhaa, Drenthe
alidai mara ya mwisho alipokutana uwanjani na Messi, pia aligoma kupeana naye
mikono baada ya mechi.
Jana, Ligi Kuu ya Hispania, Primera Liga ilisema
haijapanga kumchukulia hatua Messi.


.png)
0 comments:
Post a Comment