Roberto Di Matteo
KOCHA wa muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo
amehakikishiwa jana kuwa uamuzi juu ya nafasi yake katika klabu huio utafanywa
baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kuna tetesi kuwa, kocha huyo wa muda amekua
na unyonge kutokana na hisia kwamba atapigwa chini na badala yake wamtafute mtu niwngine, hata ikiwa matokeo ya
mechi dhidi ya Bayern Munich yatakua mazuri.
Lakini akizungumza kwenye sherehe ya
uzinduzi wa ushirika wa klabu hio na timu ya magari ya mbio za Langalanga ya
Sauber, Mkurugenzi mtendaji Ron Gourlay ameliambia shirika la habari Press
Association kua, Klabu hio ina imani kubwa na Kocha huyo tangu ajiunge nao kama
meneja wa mda na kwamba watafanya tathmini yao mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, Gourlay alishindwa kujibu kama
Di Matteo amefanya kazi ya kutosha kuwekwa kwenye orodha ya wagombea wa nafasi
ya Meneja wa klabu.
Hata kabla ya kufuzu kushiriki fainali ya
Ligi ya mabingwa, mashabiki wengi walimuunga mkono Di Mateo achaguliwe kumrithi
Andre Villas Boas.
Licha ya imani zote hizo, endapo Di Mateo
atashindwa kuwika mjini Muinich,basi Abramovich ataitumia kama sababu ya
kumuondoa Di Mateo ambaye atakua ameshindwa kuipandisha Chelsea kutoka nafasi
ya sita kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Premiership na hivyo kukosa michuano ya
Klabu bingwa barani Ulaya mwakani.


.png)
0 comments:
Post a Comment