Yaya Toure
Yaya Toure
KIUNGO wa kimatairfa wa Ivory Coast, Yaya
Toure amesema kwamba anataka kuisadia klabu yake ya Manchester City iwe klabu
bora duniani.
Mwanasoka huyo bora wa mwaka Afrika, amekua
chachu ya mafanikio ya klabu hiyo msimu huu, ambayo Jumapili inatarajiwa
kuhitimisha kwa msimu kwa taji la Ligi Kuu ya England.
Yaya amesema; “Sababu iliyonileta hapa ni
kuisadia timu.......kusaidia katika kuipeleka mbele na kuifanya iwe kubwa
kuliko zote duniani,”alisema.
City itakuwa mwenyeji wa QPR Jumapili na
ikishinda mechi hiyo itakuwa bingwa- labda Manchester United iifunge Sunderland
kwa angalau mabao 10-0.
Alipoulizwa kama ameanza kuhisi shinikizo
za pambano hilo la mwisho, Toure aliyesajiliwa kutoka Barcelona kwa kitita cha
pauni milioni 24, alijibu hapana, kwa sababu nina uzowefu. Nimeisha shiriki
michuano kama hii na kushinda vikombe kadhaa.
Toure, alikua na klabu ya Barcelona
iliyoshinda vikombe sita vya nchini na nje ya nchi mwaka 2009 na amekua
kishawishi kikubwa msimu huu kwa Manchester city.


.png)
0 comments:
Post a Comment