| Rice |
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amemsifu
msaidizi wake katika klabu hiyo, Pat Rice, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu
huu, baada ya miaka 44 akiwa na 'Gunners'.
Mrithi wake atakuwa ni mlinzi wa zamani wa
Arsenal, Steve Bould. Rice, ambaye aliichezea Arsenal katika mechi zaidi ya
500, alijiunga na wafanyikazi wa klabu ya Arsenal mwaka 1996, wakati Mfaransa
Arsene Wenger alijiunga na klabu kama meneja.
Kama meneja msaidizi, Rice aliisaidia
Arsenal kufanikiwa kupata ushindi wa ligi ya Premier mara tatu, na mara nne
kulitwaa Kombe la FA.
Meneja Wenger amesema ni vigumu kukadiria
kazi aliyoifanya Rice, na kuelezea kwamba ni jambo la "huzuni, huzuni,
huzuni sana, na binafsi namshukuru kwa mchango wake katika kunisaidia wakati
wangu na ningependa anisamehe kwa baadhi ya shida alizozipata katika kipindi
alichokuwa chini yangu, lakini alikuwa ni msaidizi mwaminufu sana, na
ninamshukuru kwa kuwa kando yangu kwa muda mrefu hivyo".


.png)
0 comments:
Post a Comment