KOCHA mpya wa timu ya soka ya taifa ya England,
Roy Hodgson ameanza kutengeneza benchi lake la ufundi, kwa kumteua kipa wa makocha
wa Birmingham City, Dave Watson kufanya kazi hiyo katika timu ya taifa kwa
ajili ya fainali za mwezi ujao za Kombe la Mataifa ya Ulaya.
England pia inataka kumrejesha kipa wa
zamani wa Liverpool na England, Ray Clemence, aliyekuwa kocha wa makipa wakati wa
Fabio Capello afanye kazi na Hodgson.
Watson, pia alifanya kazi kwa karibu na Joe
Hart wakati kipa huyo namba moja wa sasa wa England alipokuwa akicheza kwa
mkopo Birmingham msimu wa 2009/2010.
Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha
vijana cha England chini ya umri wa miaka 21, Watson alichezea klabu ya Barnsley
enzi zake, ingawa alilazimika kustaafu akiwa ana umri wa miaka 28 tu, baada ya
kuumia.
Hodgson, anayetarajiwa kutaja kikosi chake
cha Euro 2012, wiki ijayo katika michuano itakayofanyika Poland na Ukrine,
alimkaribisha Watson kwa kusema: "Dave ana thamani kubwa katika mchezo na
anaheshimika sana mbele ya makipa waliofanya naye kazi, muhimu Joe Hart.
"Amefanya kazi na makipa wengi wa England
na ana uzoefu wa kufanya kazi za maendeleo ya timu, hivyo tunafahamu atafaa
sana kwenye kikosi.
"Binafasi nafurahi kuwa naye kama
sehemu ya benchi la ufundi la England kwenye michuano hiyo. Ningependa kuwashukuru
wote katika klabu ya Birmingham City kwa kumkubalia Dave kufanya kazi katika
Euros."
0 comments:
Post a Comment