ENZI ZA RAHA ZAO; Thandi Ojeer na Claude Makelele kabla ya kuachana
| Thandi baada ya kujeruhiwa |
MLIMBWENDE wa Kiingereza, alijikuta
anapoteza uzuri wa sura yake baada ya kutandikwa makonde usoni na nyota wa
zamani wa klabu ya Chelsea ya England, Claude Makelele, Mahakama imesema jana.
Thandi Ojeer, mwenye umri wa miaka 35 — ambaye
aliishi na Mfaransa huyo kwa miaka miwili — alipigwa na kuumizwa vibaya na
kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa.
Kwa sababu hiyo anataka kulipwa fidia ya
pauni 70,000 kutoka kwa mchezaji huyo wa zamani wa Real Madird, mwenye umri wa miaka
39.
Ugomvi huo uliotokea nyumbani kwa mchezaji
huyo mwaka 2010 Jijini Paris, ambako kwa sasa anaifundisha klabu ya Paris
Saint-Germain.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyosomwa katika
mahakama ya Versailles Correction, Ojeer aliingia nyumbani kwa mchezaji huyo
baada ya kukuta geti liko wazi. Makelele, ambaye hakuwapo mahakamani, alisema
kwa kitendo hicho alishambuliwa vikali usoni na kujeruhiwa.
Ms Ojeer, mkazi wa London-ambaye ni
muandaaji wa shughuli, alihudhuria sherehe kadhaa na Makelele katika Paris Fashion
Week, lakini hakuna maelewano baina yao.
Lakini Mwanasheria wa Ojeer, alisema Makelele
alimpiga mteja wake. Stanislas Panon alisema mteja wake alihitaji tiba makini hospitali
kwa majeruhi aliyopata, ikiwemo jino na alilazimika kuwa nje ya kazi.
Wakili wa Makelele alisema kwamba “Alikuwa
anajaribu kumtoa nje ya nyumbani kwake, lakini katika kugoma wakagombana”.
Kiungo huyo hodari wa zamani, aliwaambia
Polisi kwamba alikwishaachana na mwanamke huyo na hakutaka tena kumuona nyumbani
kwake. Mwanamke huyo alisema alikwenda kuchukua nguo zake. Kesi hiyo
imeahirishwa hadi mwezi ujao.
Mwanamke mwingine wa zamani wa Makelele, mwanamitindo
wa M&S, Noemie Lenoir, alijaribu kujiua mapema mwaka 2010.


.png)
0 comments:
Post a Comment