• HABARI MPYA

    Friday, September 07, 2012

    CHELSEA YAWANOA MAKINDA WA TANZANIA LEO

    Sylvester Marsh

    Na Prince Akbar
    MAKOCHA watano wa klabu ya Chelsea ya England, mabingwa wa Ulaya, leo wanatarajiwa kuanza kutoka mafunzo kwa timu ya kombaini ya Copa Coca Cola Afrika, ambayo ndani yake ina wachezaji wawili wa Kitanzania nchini Afrika Kusini.
    Mafunzo hayo yatakayotolewa na Robert Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation yatafikia tamati kesho na wachezaji wataungana na timu zao kurejea nyumbani keshokutwa.
    Wachezaji wawili wa Tanzania wamechaguliwa kwenye kombaini ya kambi hiyo (Dream Team), ambao ni mfungaji bora Basil Seif ambaye ana mabao sita na kipa bora Tumaini Baraka, wakati Sylvester Marsh wa Tanzania amechaguliwa kuwa kocha bora katika kambi hiyo.
    Tanzania ilishika nafasi ya pili katika kambi ya kimataifa ya michuano hiyo inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini, kwa kufikisha pointi 14, baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Malawi katika mechi yake ya mwisho juzi, hivyo kufikisha pointi 14.
    Zambia ndiyo iliyokamata nafasi ya kwanza kwa kufikisha pointi 15 katika mechi hizo zilizochezwa kwa mtindo wa ligi baada ya nchi nyingine kushindwa kwenda Afrika Kusini kutokana na kuchelewa kupata viza.
    Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zilizowahi kambi hiyo ni Kenya, Uganda, Nigeria, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na timu mchanganyiko katika kambi hiyo (CEWA).
    Katika mechi zake Tanzania ilitoka suluhu na Nigeria, ikafungwa 3-2 na Kenya, ikaichapa Zimbabwe 3-0, ikailaza CEWA 3-0, ikaifunga Msumbiji 2-0, ikashinda 2-0 dhidi ya Uganda na ikafungwa 1-0 na Zambia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAWANOA MAKINDA WA TANZANIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top