• HABARI MPYA

    Monday, December 03, 2012

    AZAM WATUA KAMPALA KUSAKA SAINI, OKWI...

    Okwi katika Challenge ya mwaka huu

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    AZAM FC wametuma mwakilishi wao hapa kufuatilia wachezaji katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Masahariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayoendelea mjini hapa tangu Novemba 24, hadi Desemba 8, mwaka huu.
    Mwakilishi huyo alitua hapa jana na kuanzia leo ataanza kufanya kilichomleta mjini hapa.
    Rasmi Azam inakuwa klabu ya pili kutuma mwakilishi wake hapa baada ya El Merreikh ya Sudan.
    Mapema mwanzoni mwa mashindano haya, ilielezwa wawakilishi wa Simba, Yanga na Coastal Union watakuja pia hapa kutazama vipaji vya kuongeza katika klabu zao, lakini hadi jana hakukuwa na taarifa za mwakilishi yoyote wa klabu hizo kufika hapa.
    Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Bin Slum ilielezwa atatua leo sawa na Seif Ahmad ‘Seif Magari’, Abdallah Ahmad Bin Kleb wa Yanga na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wa Simba.
    Kiongozi wa zamani wa Simba SC, Alhaj Juma Nkamia, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini yeye tayari yupo hapa kwa wiki nzima, lakini ameletwa na mapenzi yake kwa timu yake ya taifa.
    Kuna wasiwasi, mmoja wa wachezaji ambao Azam imekuja kuwatazama huku ni mshambuliaji wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi ambaye inadaiwa mkataba wake umemalizika, ingawa klabu yake imesema unaisha Mei mwakani.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM WATUA KAMPALA KUSAKA SAINI, OKWI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top