• HABARI MPYA

    Wednesday, December 05, 2012

    BEKI STARS YAMVUNJA NGUVU OKWI

    Okwi

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    EMANUEL Okwi, mshambuliaji tegemeo wa Uganda, amesema kwamba ukuta wa Tanzania Bara ni mzuri na kuupita ni kazi, lakini akaapa kesho watafanya kila wawezalo kuhakikisha wanaupenya na kufunga.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Okwi alisema kwamba wachezaji wote wa safu ya ulinzi ya Stars wana akili na nguvu za kupambana na mshambuliaji wa aina yeyote, hivyo keso itakuwa kazi sana.
    “Inahitaji maarifa sana kuweza kupenya pale, Shomary (Kapombe) ni mchezaji mwenye akili sana na anajituma, Yondan (Kevin), pia ana akili sana, uzoefu na anajituma. Mimi nimemkuta pale Simba hadi anahamia Yanga (msimu huu).
    Na tangu nakuja Simba yeye ni mchezaji wa timu ya taifa, wana Kaseja (Juma) kipa mzuri na mzoefu, tena sana, kwa hivyo ukuta wao ni mzuri sana, ila na sisi tuna safu kali sana ya ushambuliaji, Diego (Hamisi Kiiza), Brian (Umony), Ssentongo (Robert), Kizito (Geoffrey) na mimi, wote nadhani unajua cheche zetu.
    Kwa hivyo hiyo mechi itakuwa sana, lakini sisi kwa sababu tunacheza nyumbani, inatupa nafasi nzuri zaidi ya kusonga mbele, yote kwa yote, mchezo utakuwa mgumu, ila kushinda sisi lazima,”alisema Okwi.
    Wakati ukuta wa Cranes haujaruhusu hata bao moja, ukuta wa Stars umeruhusu bao moja tu katika mechi nne, dhidi ya Burundi, tena la penalti lilofungwa na Nahodha wao, Suleiman Ndikumana, Kilimanjaro Stars ikilala 1-0.         
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BEKI STARS YAMVUNJA NGUVU OKWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top