![]() |
Kipa wa Pirates |
KOCHA wa Orlando Pirates,
Augusto Palacios amesema kwamba mashabiki waliomzomea kipa Senzo Meyiwa Jumatatu
hawana aibu.
Meyiwa, ambaye alichukua nafasi
ya Moeneeb Josephs, alizomewa kwa kufungwa bao la mbali la kiungo wa Jomo
Cosmos, Siyabonga Nhlapho ingawa timu yake ilishinda 2-1 dhidi ya Ezenkosi katika
mechi ya Ligi Kuu Uwanja wa Orlando.
Kocha huyo raia wa Peru amesema aibu
ni kwamba mashabiki wa Pirates wanamzomea mchezaji wao wenyewe.
"Kitu kimoja ambacho sikukupenda
kwenye mechi hiyo ilikuwa ni jinsi mashabiki walivyopmfanyia Senzo,”alisema.
0 comments:
Post a Comment