![]() |
Ngassa alipokuwa Marekani |
KLABU ya Chelsea itacheza na
nyota wa Ligi Kuu ya soka ya Marekani, MLS All-Stars huko Philadelphia, Julai
25, mwaka huu, ikiwa sehemu ya ziara klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England nchini
Marekani.
All-Star ya MLS ilimenyana na
mabingwa wa England, Manchester United mara mbili miaka miwili iliyop-ita. Chelsea
ilicheza na All-Stars hiyo mwaka 2006.
Chelsea itacheza mechi nyingine
na Seattle Sounders Julai 18, mwaka huu.
Mchezaji wa zamani wa kimataifa
wa Poland, Peter Nowak atachezea MLS All-Stars kwenye Uwanja wa PPL Park –
nyumbani kwa timu ya Philadelphia Union, ambayo hivi karibuni ilimtema kiungo
Mtanzania, Nizar Khalfan.
Mwaka jana, mshambuliaji wa
Tanzania Mrisho Ngassa alipewa katika 10 kuichezea Seattle Sounders mechi ya
kirafiki dhidi ya Manchester United, wakati Nizar akiwa bado Vancouver
Whitecaps aliichezea katika mechi na Manchester City.
0 comments:
Post a Comment