• HABARI MPYA

    Friday, May 11, 2012

    AL SHABAAB WAVAMIA YANGA, WAFANYA VURUGU KUBWA


    Makao makuu ya Yanga

     Baadhi ya wanachama wa Yanga wakifanya fujo klabuni hapo kupinga mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa ufanywe na mwenyekiti wa klabu hiyo Bw. Loyd Nchunga leo mchana ambapo polisi walifika klabuni hapo na kuimarisha ulinzi hadi Fullshangweblog inaondoka klabuni hapo bado kulikuwa na kundi la wanachama na kila moja akiongea la kwake na mkutano ulikuwa bado kufanyika.
     Mmoja wa askari akimuondoa mmoja wa wanachama wa klabu hiyo katika eneo lililokuwa na vurugu klabuni hapo.
     Polisi wakiwa katika magari yao tayari kabisa kuzuia vurugu endapo zingezuka klabuni hapo.
    Moja wa magari ya polisi likiwa limeegeshwa nje ya klabu hiyo kwa ajili ya kulinda usalama klabuni hapo leo mchana

    WATU wanaosadikiwa kutumwa na wapinzani wa Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Lloyd Bahargu Nchunga wamevamia makao makuu ya klabu, kuvuruga Mkutano wa Mwenyekiti huyo na Waandishi wa Habari mchana huu.
    Watu hao wanadaiwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
    Nchunga aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari wa saa 5:00 asubuhi ya leo, kuelelezea yale yaliyofikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji jana.
    HIZI NI TAARIFA ZA AWALI, HABARI KAMILI INAKUJA.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL SHABAAB WAVAMIA YANGA, WAFANYA VURUGU KUBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top