• HABARI MPYA

    Saturday, May 05, 2012

    OKWI ASAJILI BEKI NA KIUNGO SIMBA SC



    Emmanuel Okwi
    MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema kama angepewa jukumu la kufanya usajili kwenye kikosi hicho, angeongeza wachezaji wawili wapya, mmoja kwenye nafasi ya beki na mwingine kiungo.
    Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti la leo, Okwi ndiye alikuwa nyota wa mchezo dhidi ya Al-Ahly Shandy ya Sudan uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi Jumapili na Simba kushinda mabao 3-0.
    "Naamini kwa sasa tatizo kwenye kikosi cha Simba lipo kwenye nafasi ya beki wa kati na kiungo," alisema Okwi mwenye mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara sawa na Kenneth Asamoah wa Yanga na Nsa Job wa Villa Squad.
    Alifafanua kuwa nafasi ya beki wa kati imekuwa ikiyumba pale inapotokea mmojawapo ameumia ama kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.
    "Mwalimu hulazimika kumtoa Kapombe (Shomari) beki wa kulia na kumrudisha kuziba nafasi hiyo kama ulivyoona kwenye mchezo wa leo (juzi Jumapili)," alisema raia huyo wa Uganda.
    Alisema kwa sasa kikosi hicho kinahitaji kiungo mkabaji kama alivyokuwa Mkenya Jerry Santo.
    Alisema: "Hatuna kiungo ambaye anaweza kucheza kama alivyokuwa Santo (Jerry)."
    Simba ilimrudisha beki wa kati wa Uganda, Derrick Walulya, ambaye ameshindwa kuonyesha makali yake kwenye kikosi hicho na mara nyingine amekosa hata namba ya kupumzika benchi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI ASAJILI BEKI NA KIUNGO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top