Getty
KIUNGO wa Chelsea, Ramires amesema kwamba kurejea
kwa makali ya kufunga mabao kwa Fernando Torres ni moja kati ya mambo mazuri
juu ya klabu hiyo kwa sasa.
Mspanyola huyo alipiga hat trick Jumapili
katika ushindi wa 6-1 dhidi ya QPR kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na mchezaji
mwenzake wa Kibrazil ameelezea furaha yake juu ya kuzinduka kwa mshambuliaji
huyo wa zamani wa Liverpool.
“Kitu kizuri kuhusu Chelsea? Kujiamini
kwetu kumeongezeka na tuna Fernando Torres anayefunga tena," Ramires alisema.
“Sasa tunaweza kumfunga yeyote na tumeonyesha hilo Camp Nou [katika fainali ya
Ligi ya Mabingwa kuifunga Barcelona].”
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ataikosa
fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa sababu ya kutumikia adhabu ya kazi na amesema
kwamba mechi ya fainali ya Kombe la FA leo dhidi ya Liverpool itadhihirisha
makali yake.
“Kwangu, ni mechi ya msimu, kwa sababu sitacheaza
fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Munich na ninataka kushinda taji msimu huu,"
alisema.
0 comments:
Post a Comment