![]() |
| Mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC |
KLABU ya African Lyon imenusurika kushuka
daraja, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja
wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Lyon imetimiza pointi 27 na kuungana na Polisi Dodoma,
Villa Squad na Moro United kuiaga Ligi Kuu.
Villa Squad jana iliifunga 2- 1 Ruvu
Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi na kumaliza ligi na pointi 26 sawa
na Toto Africans iliyofungwa bao 1-0 na Coastal Union jana Uwanja wa Mkwakwani
Tanga.
Mtibwa Sugar ilimaliza vizuri, baada ya kuifunga
Moro United bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, hivyo Mtibwa kumaliza ligi
ikiwa na pointi 42.
Jana Simba ilitawazwa rasmi kuwa mabingwa
wapya wa Ligi Kuu, baada ya kuifunga Yanga mabao 5-0 na kumaliza ikiwa na
pointi 62.
Simba ilipata mabao yake kupitia kwa,
Emmanuel Okwi dakika ya kwanza na Patrick na 65, Mafisango dakika ya 58 kwa penalti,
Juma Kaseja kwa penalti pia dakika ya 69 na
Felix Sunzu kwa penalti dakika ya 74.
Wakati Simba ikimaliza na pointi zake 62, Azam
imekuwa ya pili kwa pointi zake 56 baada ya jana kuifunga Kagera Sugar mabao
2-1 Uwanja wa Chamazi na Yanga imeshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 49.



.png)
0 comments:
Post a Comment