![]() |
| Azam wako Moshi leo |
Na Mahmoud Zubeiry
MICHUANO ya BankABC Sup8r inatarajiwa kuendelea leo kwenye
viwanja vinne nchini, kwa michezo minne ya kukamilisha hatua ya makundi.
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kocha Suleiman Abdallah
Matola ataiongoza Simba B katika mechi dhidi ya Zimamoto FC ya Zanzibar, wakati
Uwanja wa Chamazi, Jamhuri FC itakuwa mwenyeji wa Mtende, zote za Zanzibar.
Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Kocha Mecky Mexime ataiongoza
Mtibwa Sugar katika mchezo dhidi ya wenyeji Super Falcon FC, wakati Uwanja wa
Ushirika mjini Moshi, Azam FC watapepetana na Polisi Moro FC.
Katika Kundi A, Simba SC inaongoza kwa pointi zake nne,
baada ya kutoa sare moja na kushinda moja, ikifuatiwa na Zimamoto na Mtende
zinazofungana kwa pointi tatu kila moja, wakati Jamhuri inashika mkia kwa
pointi yake moja.
Kundi B, Mtibwa inaongoza kwa pointi zake sita ikifuatiwa na
Azam FC na Polisi Moro, zenye pointi tatu kila moja, wakati Falcon inashika
mkia, ikiwa haina pointi hata moja.
Wakati hatua ya makundi inamalizika leo, mechi za Nusu
fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam. Mdhamini wa michuano hiyo,
Banc ABC anagharamia usafiri wa ndege kwa timu zote kutoka kituo kimoja hadi
kingine, malazi na jezi.
Kanuni za mashindano haya ni kushirikisha timu zilizoshika
nafasi tatu za juu katika Ligi Kuu za Bara na visiwani na mbili zilioongoza
katika kupanda Ligi Kuu zote mbili, lakini kwa Bara, Yanga waliokuwa washindi
wa tatu msimu uliopita, walijitokea na nafasi yao ikachukuliwa na Mtibwa Sugar
ambayo ilishika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu.
Bingwa wa michuano hiyo mipya itakayokuwa ikifanyika kila
mwaka, ataondoka na Sh. Milioni 40, mshindi wa pili Sh. Milioni 20, wa tatu Sh.
Milioni 15 sawa na wa nne, wakati washiriki wengine wataondoka na Sh. Milioni 5
kila moja.
KUNDI A
P W D L GD P
Simba B 2 1 1 - 1 4
Zimamoto 2 1 - 1 1 3
Mtende FC 2 1 - 1 -1 3
Jamhuri FC 2 - - 1 -2 1
MATOKEO/RATIBA
Agosti 5, 2012
Simba SC 1-1 Jamhuri FC
Zimamoto FC 2-3 Mtende FC
Agosti 9, 2012
Jamhuri FC 0-2 Zimamoto FC
Mtende FC 0-2 Simba SC
Agosti 12, 2012
Simba SC vs Zimamoto FC
(Saa 10:00 jioni, Mwanza)
Jamhuri FC vs Mtende FC
(Saa 10:00 jioni, Chamazi)
KUNDI B
P W D L GD P
Mtibwa 2 2 - - 3 6
Azam FC 2 1 - 1 2 3
Polisi Moro 2 1 - 1 1 3
S. Falcon 2 - - 2 -4 0
MATOKEO/RATIBA
Agosti 5, 2012
Super Falcon FC 0-2 Azam FC
Agosti 6, 2012
Mtibwa Sugar FC 2-1 Polisi Moro FC
Agosti 9, 2012
Azam FC 0-2 Mtibwa Sugar FC
Polisi Moro FC 2-0 Super Falcon FC
Agosti 12, 2012
Super Falcon FC vs Mtibwa Sigar FC (Saa 2:00 usiku, Z’bar)
Azam FC vs Polisi Moro FC (Saa10:00
jioni, Moshi)



.png)
0 comments:
Post a Comment