• HABARI MPYA

    Monday, August 06, 2012

    BWAWA LIMEINGIA RUBA, YANGA TAYARI WAPO KWA OKWI, AZAM NAO WAMO

    Okwi

    Na Mahmoud Zubeiry
    EMMANUEL Okwi, wakati wowote anaweza kutangazwa kuwa mchezaji mpya wa Yanga, ingawa Azam FC nao baada ya kukerwa na kitendo cha Simba kumsainisha Ramadhan Chombo ‘Redondo’ nao wanamsaka wamsainishe kulipa kisasi.
    Hivi unaposoma habari hii, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb yupo mjini Kampala, Uganda akishughulikia suala la mchezaji huyo wa kimataifa wa Uganda.
    “Ndio, nipo Uganda, nipo Kampala hivi sasa, nakubali Rage (Ismail Aden, Mwenyekiti wa Simba), alinizidi maarifa Kigali (Rwanda) katika usajili wa Mbuyu Twite, ila sasa na mimi nataka kulipa kisasi, we subiri tu muda si mrefu utapata habari,”alisema Bin Kleb, alipozungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu dakika chache zilizopita kutoka Kampala.
    Alipoulizwa ni kuhusu mchezaji gani, Bin Kleb alikataa kumtaja, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu kwa sasa hakuna mchezaji ambaye Simba wanamfuatilia Uganda, zaidi ya mchezaji wao tu, Okwi ambaye alikuwa Ulaya kwa majaribio ambako amefeli.
    Wiki iliyopita, Alhaj Rage alimzidi kete Bin Kleb mjini Kigali, Rwanda katika kumuwania beki wa APR ya huko, Mbuyu Twite, ambaye amesaini miaka miwili na SImba SC.
    Okwi, licha ya awali kuelezwa kwamba amefuzu majaribio katika klabu ya FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim, Austria, lakini mwishoni mwa wiki ilielezwa kwamba, klabu hiyo haitamnunua tena, baada ya wiki tatu za kuwa nchini humo akijaribiwa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BWAWA LIMEINGIA RUBA, YANGA TAYARI WAPO KWA OKWI, AZAM NAO WAMO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top