![]() |
| Mh Misanga akitambulisha Tawi la Yanga Bungeni, kulia kwake ni Manji, Martha na Mkuchika na kushoto na Mama Karume na Kifukwe |
Na Mahmoud Zubeiry
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambao ni wapenzi wa
Yanga watakuwa wakichangia Sh. 500,000 kila mwaka katika kuchangia maendeleo ya
klabu hiyo, hayo yamefikiwa leo katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma,
wakati wa hafla ya fupi ya uzinduzi wa Tawi la Yanga Bungeni.
Hiyo ilifuatia ombi la Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la
klabu ya Yanga, Mama Fatuma Karume, mke wa rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati
Abeid Amaan Karume leo wakati akizindua tawi la Yanga Bungeni.
Mama Karume alizindua mfuko huo kwanza yeye mwenyewe kutoa
Sh. 500, 000 ambazo zilipokewa na Mweka Hazina wa Tawi la Yanga Bungeni, Martha
Moses Mlala, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Singida.
Wabunge wengine waliotoa fedha zao hapo hapo ni Abbas Mtemvu
(Temeke, CCM). Athumani Mfutakamba (Igalula, CCM) na Grace Kiwelu (Viti Maalum,
CCM).
Awali, akisoma taarifa ya tawi hilo, Mwenyekiti Misanga
ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga miaka ya 1970, chini ya Mwenyekiti
Juma Shamte, alisema kwamba Julai 31 walifanya uchaguzi wa viongozi wa tawi la
klabu hiyo Bungeni na mbali ya yeye kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, Abadallah Ameir
alichaguliwa kuwa Makamu wake.
Alisema Nafasi ya Katibu Mkuu, ilikwenda kwa Godfrey Zambi,
Katibu Msaidizi, Grace Kiwelu, Mweka Hazina Martha Mlala na Wajumbe wa Kamati
ya Utendaji, Abbas Mtemvu, Halima Mdee, Victor Mwambalaswa, Mohammed Chambo,
Abdul Marombwa, Vicky Kamatta na Ritta Kabati.
Aidha, alisema waliteua pia Kamati ya Ushauri ya Wajumbe wanne,
ambao ni George Mkuchika, Zarina Madabida, Faki Makame na Chirtopher Chiza.
Pamoja na hayo, Misanga aliupongeza uongozi mpya wa Yanga
chini ya Mwenyekiti wake Manji, na kuutaka uwe makini na wanachama wapandikiza
sumu za migogoro klabuni.
Tawi hilo jipya la Yanga, limepanga kuwafuturisha wachezaji
wa Yanga jioni ya leo, kabla ya kurejea Dar es Salaam.
![]() |
| Martha akihesabu michango ya Wabunge wenzake |
![]() |
| Mh Zambi kulia akifungua kikao |
![]() |
| MAKOCHA; Kutoka kulia ni Tom, Minziro na Samatta |
![]() |
| Waheshimiwa Yanga damu |
![]() |
| Tegete na Chuji |
![]() |
| WALIOTOKEA SIMBA KIVYAO; Kutoka kulia Gumbo, Barthez na Yondan |
![]() |
| Mh Mtemvu, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe katika utambulisho wa Tawi la Yanga Bungeni |
![]() |
| Meza kuu |
![]() |
| Manji na Misanga |













.png)
0 comments:
Post a Comment