Na Mahmoud Zubeiry
AZAM FC imesema kwamba, Simba SC imekurupuka kumsajili kiungo
Ramadhani Suleiman Chombo ‘Redondo’, bila kuwasiliana na klabu yake na
yatawatokea kama yaliyowatokea kwa Ibrahim Rajab ‘Jeba’, kupoteza fedha zao
walizompa mchezaji.
Kiongozi mmoja wa Azam, ameiambia BIN ZUBEIRY sasa hivi
kwamba, wanasikia tetesi leo Redondo amesajiliwa
Simba SC, lakini mchezaji huyo bado ana mkataba na Azam hadi Juni mwakani.
“Redondo alikuwa hajui mkataba wake unamalizika lini Azam, alinifuata
kuniomba nimuongezee fedha asaini mkataba mpya, nikamuahidi nitafanya hivyo,
lakini baadaye nakuja kugundua mkataba wake unaisha Juni mwakani, nikamuambia
asubiri angalau baada ya miezi miwili.
Kwa sababu haiwezekani umpe mtu fedha wakati mkataba wake
bado muda mrefu kiasi hiki, sasa ajabu amekwenda kusaini Simba, “alisema kwa
kustaajabu kiongozi huyo.
Habari za uhakika kutoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi zimeithibitishia
BIN
ZUBEIRY kwamba Redondo amesaini Simba. Kiungo huyo aliyejiunga na Azam
mwaka 2009, akitokea Simba anakuwa mchezaji wa pili ndani ya kipindi kisichozidi
siku tano kutua Msimbazi, akitokea Azam, baada ya Jumatano iliyopita, Mrisho
Ngassa pia kusajiliwa na timu hiyo akitokea Chamazil.
Alipoulizwa Ofisa Habari wa Smba SC, Ezekiel Kamwaga alisema
kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sasa.
Simba ilimsajili mshambuliaji chipukizi wa Azam, Jeba
aliyekuwea akicheza kwa mkopo Villa Squad kwa kuamini hana mkataba na klabu
yake, lakini baadaye ililazimika kumsalimisha mchezaji huyo baad aya kugundua
ana mkataba na Azam.



.png)
0 comments:
Post a Comment