• HABARI MPYA

    Friday, August 10, 2012

    DULLAH MABAO WA MSIMBAZI SASA 100%


    Dullah kujlia akimtoka Shikanda wa Azam
    Na Prince Akbar
    MSHAMBULIAJI chipukizi wa Simba SC, Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’, amesema kwamba hivi sasa yuko fiti kabisa baada ya kuumia kwenye mechi za makundi za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Dullah alisema kwamba anamshukuru Mungu amepona na anaendelea vizuri na mazoezi.
    “Niko fiti, naendelea vizuri, nadhani hadi kuja kuanza kwa ligi, mashabiki watashangilia sana mabao na mimi, tumuombe Mungu kaka,”alisema Dullah.
    Dullah aliingia akitokea benchi juzi katika mechi dhidi ya City Stars ya Nairobi na awali akicheza pembeni alicheza vizuri, kwa sababu alikuwa anahaha kuwatengenezea nafasi za kufunga wenzake.
    Lakini alipohamishiwa ndani, alijikuta hana cha kufanya kutokana na safu yote ya kiungo ya Simba ‘kufa’ na kushindwa kumlisha mipira. Katika mchezo huo, Simba ilifungwa mabao 3-1, ikitoka kuongoza kwa 1-0 hadi mapumziko.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DULLAH MABAO WA MSIMBAZI SASA 100% Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top