Tetesi za Jumatatu magazeti Ulaya
FERGUSON AACHA KILA KITU MAN UNITED KUSHUGHULIKIA USAJILI WA VAN PERSIE
Sir Alex Ferguson aliikosa mechi ya sare ya bila kufungana ya Manchester United na Valerenga jana, kwa sababu alikuwa anashughulikiwa usajili wa Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie, 28.
Ferguson ameamua kufanya kweli sasa katika kuwania saini ya Van Persie, baada ya kocha wa Manchester City, Roberto Mancini kusema kwa mara ya kwanza hakutarajai kumsajili Mholanzi huyo.
Manchester United pia ina matumaini ya kuinasa saini ya kinda wa Malaga, anayechezea pia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, Isco, mwenye umri wa miaka 20, kwa kuwa klabu yake inakabiliwa na hali ngumu ya kifedha hivi sasa.
Beki wa Chelsea, Ashley Cole, mwenye 31, amefuta mpango wa kuhamia kwa matajiri wa Ufaransa, Paris Saint Germain ingawa amesema mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake ya Stamford Bridge bado hayajafanyika.
Liverpool iko hatarini kuikosa saini ya Clint Dempsey, mwenye umri wa miaka 29, kutokana na kocha Brendan Rodgers kuonyesha kutovutiwa na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Marekani na Fulham mwenye thamani ya pauni Milioni 10.
Nottingham Forest inataka kumsajili beki kinda wa Norwich City, anayechezea timu ya taifa ya vijana ya Hispania, Dani Ayala kwa mkopo wa muda mrefu.
Tottenham inaangalia mchezaji mwihgine wa kumsajili baada ya mshambuliaji mwenye umri wa 22 wa Malaga, Salomon Rondon, waliyekuwa wanamtaka awali, kuwa mbioni kujiunga na Rubin Kazan ya Urusi.
PIENAAR AWACHOKOZA MAN UTD
Mchezaji mpya wa Everton, Steven Pienaar, mwenye umri wa miaka 30, amemtaka Leighton Baines kubaki The Toffees wakati beki huyo wa kushoto akiendelea kuhusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United.
NYOTA wa Real Madrid na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 27, amesema angependa kufuata nyayo za David Beckham kucheza Marekani katika Ligi Kuu ya huko, atakapomaliza Hispania.
Mchezaji mpya wa Arsenal, Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25, anaamini klabu yake mpya inaweza kufufua makali na kumfanya kuendelea kuwa mshindi wa mataji kama ilivyokuwa Ufaransa. Arsene Wenger alimsajili Giroud kutoka Montpellier, ambako mshambuliaji huyo alikuwa miongoni mwa timu iliyoipiku Paris Saint Germain katika mbio za taji la Ligue 1.
Full story: talkSPORT
HUGHES KUREJEA UWANJANI
Mtaliano mmiliki wa mgahawa, Richard Hughes, mwenye umri wa miaka 33, amesema anataka kurejea uwanjani kwa kujiunga na Bournemouth kwa mkataba wa miaka miwili.


.png)
0 comments:
Post a Comment