• HABARI MPYA

    Monday, August 06, 2012

    REDONDO ASAINI SIMBA LEO

    Kiungo Ramadhan Suleiman Chombo ‘Redondo’ leo amesajiliwa Simba SC, akitokea Azam FC katika mkataba ambao bado haujaeleweka, lakini habari za uhakika kutoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi zimeithibitishia BIN ZUBEIRY hivyo. Kiungo huyo aliyejiunga na Azam mwaka 2009, akitokea Simba anakuwa mchezaji wa pili ndani ya kipindi kisichozidi siku tano kutua Msimbazi, akitokea Azam, baada ya Jumatano iliyopita, Mrisho Ngassa pia kusajiliwa na timu hiyo akitokea Chamazil. BIN ZUBEIRY bado inafuatilia kwa kina kujua aina ya mkataba ambao Redoindo wa Keko Magurumbasi amesaini na Simba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REDONDO ASAINI SIMBA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top