• HABARI MPYA

    Wednesday, August 08, 2012

    MJUE MILIONEA ALIYEWASAJILI SUNZU, NGASSA SIMBA SC

    Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ni Makamu Mwenyekiti wa Simba na wengi wanajua mchango wake katika klabu, akiwa anatoa fedha nyingi kwenye akaunti zake kusajili wachezaji na kufanya mambo mengine kadhaa.
    Lakini ndani ya Simba SC, kuna watu wengine ambao wanajitolea mno kusaidia timu, kama au zaidi ya Kaburu. Miongoni mwao ni huyu mtu pichani, anaitwa Zakaria Hans Pop, ambaye hivi karibuni amefungua akaunti zake kumsajili Mrisho Khalfan Ngassa kutoka Azam FC.
    Huyu jamaa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, kwa fedha yake pia ndiye aliyemsajili mshambuliaji Mzambia, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasika ya Kongo (DRC), Felix Mumba Sunzu Jr kutoka El Hilal ya Sudan. Katika Simba Dar, hii ndio zawadi ya BIN ZUBEIRY kwa wana Simba SC.  


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MJUE MILIONEA ALIYEWASAJILI SUNZU, NGASSA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top