![]() |
Simba wakiwapungia mikono mashabiki kabla ya mechi |
Na Mahmoud Zubeiry
SIMBA SC imefungwa mabao 3-1 na Nairobi City Stars katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika mechi iliyochezwa sambamba na
Simba Day.
Lakini kufungwa huko kwa Simba kulitokana na kocha Milovan Cirkovick
kubadilisha karibu kikosi kizima kilichoanza na kuingiza wachezaji wapya, ambao
waliitoa City Stars ya Nairobi nyuma kwa 1-0 na kuipa ushindi wa 3-1.
Simba ilitangulia kupata bao kupitia kwa Felix Sunzu dakika
ya 15, pasi ya Mwinyi Kazimot na ilikwenda kupiumzika ikiwa mbele kwa bao hilo.
Lakini kipindi cha pili, kipa aliyempokea Juma Kaseja,
Hamadi Waziri alitunguliwa mabao matatu katika dakika 57 na Duncan Owiti,
dakika ya 64 na Bruno Okullu na dakika ya 79 na Boniphace Onyango.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Simba, Milovan alisema kwamba
alibadilisha kikosi kizima kipindi cha pili, kwa sababu alitaka awaone
wachezaji wote uwezo wao.
Alipoulizwa kuhusu muda uliobaki kabla ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kuanza, kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam mwishoni mwa
mwezi huu, Milo alisema muda unatosha na atakuwa kikosi tishio.
“Nina wachezaji wazuri wengi, hujamuona Kapombe uwanjani
leo, muda unatosha sana,”alisema Milovan, raia wa Serbia.
Mapema katika tamasha hilo, Simba ilitoa tuzo mbalimbali kwa
wachezaji wa sasa na wa zamani kwa mchango wao kwenye klabu hiyo, pamoja na
baadhi ya wadau wake.
Waliopewa tuzo kwa wachezaji wa sasa, ni Shomary Kapombe
(Nidhamu), Emmanuel Okwi (Mchezaji bora wa msimu) na marehemu Patrick Mfisango
(Heshima).
Wa zamani ni Haidari Abeid ‘Muchacho’ (Mchezaji Bora miaka
ya 1970), Hamisi Kilomoni (Mchezaji Bora Miaka ya 1960), Ally Sykes (Heshima,
Udhamini), Profesa Philemon Sarungi (Mchango wa muda mrefu klabuni) na Gaorge
Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer, Wadhamini wa sasa wa Simba SC.
Katika mechi ya kwanza, timu na wanawake ya Simba, Simba
Queens mchana wa leo, iliifunga Ever Green ya Temeke mabao 5-3 katika mchezo wa
Ligi ya Wanawake, Dar es Salaam uliokwenda sambamba na tamasha la Simba Day,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shujaa wa Simba leo, alikuwa ni Maimuma Hamisi ‘Ronaldo’ aliyefunga
mabao matatu, katika dakika za tano, 62 na 64, wakati mabao mengine ya Malkia
wa Msimbazi, walio chini ya kocha Anthony Makunja, yalifungwa na Grace Tony
dakika ya 48 na Neema Kuga dakika ya 59.
Mabao ya Ever Green yalifungwa na Sherida Boniface dakika ya
53, Vumilia Maarifa dakika ya 55 na Amina Siraj dakika ya 61.
![]() |
Ngassa baada ya kukosa bao |
![]() |
Boban kazini |
![]() |
Ngassa anatia krosi |
![]() |
Uhuru anakwatuliwa |
![]() |
Uhuru anakwepa kwanja... |
![]() |
Kikosi cha Simba; juu ndio walioanza na waliowekewa OUT maana yake walitoka, wakaingia waliowekewa IN chini |
![]() | |
|
0 comments:
Post a Comment