• HABARI MPYA

    Wednesday, August 08, 2012

    SIMBA DAY ILIVYOFANA TAIFA LEO

    KATIKA Simba Day, klabu ya Simba leo imetoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wa sasa na wa zamani kwa mchango wao kwenye klabu hiyo, pamoja na baadhi ya wadau wake.
    Waliopewa tuzo kwa wachezaji wa sasa, ni Shomary Kapombe (Nidhamu), Emmanuel Okwi (Mchezaji bora wa msimu) na marehemu Patrick Mfisango (Heshima).
    Wa zamani ni Haidari Abeid ‘Muchacho’ (Mchezaji Bora miaka ya 1970), Hamisi Kilomoni (Mchezaji Bora Miaka ya 1960), Ally Sykes (Heshima, Udhamini), Profesa Philemon Sarungi (Mchango wa muda mrefu klabuni) na Gaorge Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer, Wadhamini wa sasa wa Simba SC. Pichani no Okwi kushoto akipokea tuzo yake kutoka kwa Sarungi. Kulia Kavishe na nyuma ni Kaburu. PICHA ZOTE NA MAHMOUD ZUBEIRY

    Mashabiki wakionyeshana kitu

    Ujumbe kwa Katibu Mkuu wa TFF

    Kapombe akipokea tuzo yake

    Kaburu akipokea tuzo ya Mafisango 

    Mzee Kilomoni akipokea tuzo yake

    Kaburu akimkabidhi tuzo Sarungi

    Kaburu akimkabidhi tuzo Kavishe

    11 wa kwanza wa Simba msimu huu, waliosimama kutoka kulia Juma Kaseja, Juma Nyosso, Haruna Moshi, Felix Sunzu, Nassor Masoud, Uhuru Suleiman na walioinama kutoka kulia ni Haruna Shamte, Mrisho Ngassa, Amir Maftah, Salim Kinje na Mwinyi Kazimoto 

    Benchi la vifaa vitupu; kutoka kulia Amri Kiermba, Danny Mrwanda, Kiggi Makassy, Emanuel Okwi, Kanu Mbivayanga, Ramadhan Redondo, Abdallah Juma, Hamadi Waziri, Paul Ngalema na wengineo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA DAY ILIVYOFANA TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top