• HABARI MPYA

    Wednesday, August 08, 2012

    SIMBA YAUA 5-3 SIMBA DAY TAIFA

    Maimuna Ronaldo akipokea mpira baada hya kupiga 'hattrick'

    SIMBA ni moto wa kuotea mbali kuanzia soka ya vijana kwa wanaume, wakubwa hata Wabunge, mashabiki na wanawake pia. Habari ndio hiyo.
    Timu na wanawake ya Simba, Simba Queens mchana wa leo, imeifunga Ever Green ya Temeke mabao 5-3 katika mchezo wa Ligi ya Wanawake, Dar es Salaam uliokwenda sambamba na tamasha la Simba Day, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Shujaa wa Simba leo, alikuwa ni Maimuma Hamisi ‘Ronaldo’ aliyefunga mabao matatu, katika dakika za tano, 62 na 64, wakati mabao mengine ya Malkia wa Msimbazi, walio chini ya kocha Anthony Makunja, yalifungwa na Grace Tony dakika ya 48 na Neema Kuga dakika ya 59.
    Mabao ya Ever Green yalifungwa na Sherida Boniface dakika ya 53, Vumilia Maarifa dakika ya 55 na Amina Siraj dakika ya 61.
    Hivi sasa mechi kati ya Simba A na Nairobi City Stars inaingia kipindi cha pili, Felix Sunzu amekwishaifungia Simba bao dakika ya 15. Tukutane baadaye sana.
    Maimuna kushoto


    Kikosi cha Simba Queens kilichoua 5-3
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAUA 5-3 SIMBA DAY TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top