Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi
jioni hii alijimuika na Maofisa wa kampuni ya Feza, wamiliki wa shule ye Feza,
katika msikiti wao, uliopo Victoria, Dar es Salaam kupata futari. Baadhi ya Wahariri
wa Vyombo vya Habari na Waandishi, pia
walialikwa kwenye futari hiyo, akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa BIN
ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry, Mhariri wa Spoti Leo, Amir Mhando,
Mhariri wa Habari wa Habari Leo, Mgaya Kingoba, Mhariri
Mkuu wa Habari Leo, Joseph Kulangwa na mpiga picha wa magazeti ya Habari
Leo na Spoti Leo, Mohamed Mambo. Pichani ni Mzee Mwinyi kushoto akizungumza na Maofisa wa Feza kulia kwake.
|
0 comments:
Post a Comment