• HABARI MPYA

    Thursday, August 16, 2012

    WENGER: INAUMA UCHUNGU KUMPOTEZA VAN PERSIE


    KOCHA Arsene Wenger amesema kwamba Arsenal haikuwa na nguvu ya kumzuia Robin van Persie kusaini Manchester United.
    United iliipata saini ya mchezaji huyo jana usiku, baada ya Arsenal kukubali kumuuza Van Persie wapinzani wao wa taji la Ligi Kuu kwa pauni Milioni 24.
    Baada ya wiki kadhaa za majadiliano na Arsenal na mshambuliaji huyo wa Uholanzi, United imewapiku Manchester City na Juventus mbi za kuwania saini ya Van Persie mwenye umri wa miaka 29 na leo atafanyiwa vipimo vya afya Old Trafford. 
    ‘Inauma kumpoteza mchezaji wa ubora wake. Tulikuwa tumebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake, hivyo hatukuwa na chaguo,’alisema Wenger.
    In the red: How Robin van Persie will look in a Manchester United shirt in our mocked-up picture
    Hivi ndivyo Robin van Persie atakavyokuwa akionekana katika jezi ya Manchester United.

    SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER: INAUMA UCHUNGU KUMPOTEZA VAN PERSIE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top