• HABARI MPYA

    Thursday, August 16, 2012

    TFF NA KLABU KATIKA TIFU JIPYA KABLA YA LIGI KUU

    Mwesigwa

    Na Mahmoud Zubeiry
    KLABU za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinataka kukutana haraka, kujadili kile wanachodai, kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuingia mkataba mpya na wadhamini wa ligi hiyo, Vodacom Tanzania bila kuzishirikisha klabu, BIN ZUBEIRY imeambiwa.
    Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa klabu Tanzania, Celestine Mwesigwa amesema leo katika mahojiano na BIN ZUBEIRY kwamba, kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu kuna sintofahamu nyingi kutoka ndani ya TFF, likiwemo suala la udhamini.
    “Tupo katika mchakato wa kukutana klabu zote za Ligi Kuu kujadili mambo mbalimbali juu ya maslahi yetu, kubwa ni suala la udhamini, haiwezekani TFF iingie mkataba wa udhamini na Vodacom bila kutushirikisha,”alisema Mwesigwa.
    Lakini BIN ZUBEIRY, ilipowasiliana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, ambaye ni mwakilishi wa klabu ndani ya shirikisho hilo, Wallace Karia alisema kwamba bado shirikisho hilo halijaingia mkataba mpya wa udhamini wa Ligi Kuu, bali mazungumzo yanaendelea.
    “Nimesikia watakamilisha Agosti 31, na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom alimpigia simu rais wa TFF (Leodegar Tenga) akimuita kwenye kikao cha kujadili hilo suala, Tenga akaamua ili kuepusha maneno aende na Mzee Said Mohamed wa Azam, sasa waliyozungumza huko jana ndio bado sijayajua,”alisema Karia.
    Aidha, Karia aliwashutumu Yanga kwamba ndio wanakwamisha kikao cha klabu za Ligi Kuu kujadili mambo mbalimbali, kutokana na kupiga chenga kila wakiambiwa.
    Mkutano Mkuu uliopita wa TFF, uliamua kuanzia msimu ujao Ligi Kuu iendeshwe na kampuni, itakayoundwa na Klabu za ligi hiyo.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF NA KLABU KATIKA TIFU JIPYA KABLA YA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top