Tetesi za Jumanne magazeti ya Ulaya


LIVERPOOL WAIPA MAN CITY DAU


Liverpool wameiambia Manchester City kwamba beki Daniel Agger, mwenye umri wa miaka 27, atawagharimu angalau pauni Milioni 22, baada ya City kutuma maombi rasmi ya kumtaka Mdenmark huyo.
Juventus wanamtaka mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez kwa kuhofia labda Robin van Persie atakataa kujiunga nao.
Uhamisho wa Santi Cazorla kutoka Malaga kwenda Arsenal bado haujatangazwa rasmi, lakini kiungo huyo tayari ameanza mazoezi na kikosi cha Arsene Wenger katika mambi ya Ujerumani.
Lucas Moura
PSG ainapewa nafasi kubwa ya kumsaini Moura
Lucas Moura sasa inaelezwa anaweza kuhamia Paris St Germain badala ya Manchester United, baada ya kuibuka taarifa za kinda huyo wa miaka 19 kukerwa na Manchester.
Mwenyekiti wa Inter Milan, Massimo Moratti amesema kwamba wamejitoa kwenye kuwania saini ya Moura, kwa sababu PSG tayari wameipa ofa kubwa Sao Paulo kumsajili nyota huyo wa Brazil.
Jack Sullivan, mtoto wa Mwenyekiti mshiriki wa West Ham, David, ameandika kwenye Twitter dhamira ya ya klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll imekufa.
Cardiff City inakaribia kumsajili Craig Bellamy kutoka Liverpool, ingawa pia, kocha wa QPR, Mark Hughes angependa kumuongeza kwenye kikosi chake mkongwe huyo wa Wales.
Craig Bellamy
Bellamy anaweza kurejeaCardiff, alikocheza kwa mkopo msimu uliopita
Bologna inataka dau la pauni Milioni 16 kumuuza Gaston Ramirez, mwenye umri wa miaka 21, anayetakiwa na Liverpool na Tottenham. Inter Milan pia imetajwa kummezea mate kiungo huyo wa Uruguay.
Liverpool inajiandaa kwa mazungumzo ya kina na Swansea City juu ya kiungo Joe Allen sasa baada ya nyota huyo wa miaka 22 kumaliza majukumu yake kwenye michuano ya Olimpiki.
Stoke City inafanya mazungumzo na beki wa kushoto wa Poland, Sebastian Boenisch, mwenye umri wa miaka 25, ambaye yuko huru baada ya kumaliza mkataba wake Werder Bremen.

RONALDO AMFUATA BECKHAM MAREKANI

Cristiano Ronaldo amesema kwamba atafuata nyayo za winga wa zamani wa Manchester United, David Beckham kwenda kucheza Marekani baada ya kumaliza Real Madrid.