Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya

MAN UNITED YAMUAMBIA NANI AFUNGE DOMO LAKE NA AKAZANIE SOKA 

Oriol Romeu
Oriol Romeu anaweza kutimkia Valencia
Manchester United imemtaka kiungo wake, Nani, mwenye umri wa miaka 26, kuacha kuzungumzia mustakabali wake Old Trafford na kuelekeza nguvu zake katika kucheza soka.
Chelsea inapambana na jaribio la kumpoteza kiungo wake kinda wa miaka 20, Mspanyola Oriol Romeu, ambaye anatakiwa na Valencia.

HUGO LLORIS ATAKA KIKAO NA AVB

Kipa wa Tottenham, Hugo Lloris, mwenye umri wa miaka 25, yuko tayari kwa mazungumzo na kocha Andre Villas-Boas - ingawa ndio kwanza anajiunga na klabu hiyo.
Kiungo wa Southampton, Adam Lallana, mwenye umri wa miaka 24, amesema alifikiri habari za kuitwa kwake kwenye kikosi cha England ni utani wa kocha Nigel Adkins.
Kocha wa Newcastle, Alan Pardew atakabaliwa na wakati mgumu wakati wa Fainali za Kombe Januari mwakani, iwapo Senegal itaifunga Ivory Coast mwezi ujao na kufuzu kwenye fainali hizo zitakazopigwa Afrika Kusibi.

KOCHA UKRAINE AWAZUIA WACHEZAJI KUANGALIA VIDEO ENGLAND IKIUA 5-0

Kocha wa Ukraine, Oleg Blokhin amewazuia wachezaji wake kuangalia video ya mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ya wapinzani wao England, wakiifunga 5-0 Moldova.