Tetesi za Ijumaa magazeti ya Ulaya
MIROSLAV KLOSE AELEZEA JINSI ALIVYOIKATAA SPURS ABAKI LAZIO
Mshambuliaji mkongwe wa Ujerumani, Miroslav Klose, mwenye umri wa miaka 34, amesema alikataa ofa ya Tottenham Hotspur msimu huu ili abaki Lazio.
Blackpool inataka kumsajili tena mshamnbuliaji DJ Campbell kutoka QPR moja kwa moja Januari, lakini itafurahi kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30-kwa mkopo kwanza.
Manchester United inapambana na Juventus, Roma na Lazio kuwania saini ya mshambuliaji wa Sassuolo, mchambuliaji wa timu ya taifa ya vijana ya Italia chini ya umri wa miaka 19, Domenico Berardi, mwenye umri wa miaka 18.
MAKIPA MAN UNITED SASA BIFU NJE NJE
Kipa wa Manchester United, Anders Lindegaard, mwenye umri wa miaka 28, amesema upinzani wake na David de Gea, mwenye umri wa miaka 21, ni mzuri kwa timu.
Kiungo wa West Ham, Mark Noble, mwenye umri wa miaka 25, ametakiwa na kocha Sam Allardyce kumaliza mkataba wake ili aondoke kama mchezaji huru msimu ujao.
Beki wa kulia, Bacary Sagna, mwenye umri wa miaka 29, amewekwa chini na kocha Arsene Wenger, baada ya kuelezea malalamiko yake kuhusu kuuzwa kwa Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29, na Alex Song, mwenye miaka 25.
Wayne Rooney, mwenye umri wa miaka 26, ameelezea ambavyo wachezaji wa Manchester United kwanza walivyopata mshituko kwa Alex Ferguson kuwafokea, mara baada ya kuchukua taji la msimu wa 2006-07.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis amesema kocha Arsene Wenger yuko poa kama ambavyo amekuwa siku zote.
Ni rahisi kwa wachezaji wa klabu kubwa kuitwa timu ya taifa ya England, amesema kiungo wa Norwich, Jonny Howson, mwenye umri wa miaka 24.
Kocha wa Wigan, Roberto Martinez kusajiliwa kwa mchezaji wa zamani wa Latics kwa mkopo, Tom Cleverley, mwenye umri wa miaka 23, ni kwa sababu anafaa katika mfumo wa "Total Football".
JOHN HENRY AKANA
Mmiliki wa Liverpool, John Henry amekanusha madai kwamba amepanga kuuza jukwa la Boston Red Sox kwa pauni Milioni 600.


.png)
0 comments:
Post a Comment