Tetesi za Jumatatu magazeti Ulaya
NYOTA MADRID ASITA KUSAINI MKATABA MPYA KWA DILI LA KWENDA ARSENAL
Mshambuliaji Adrian Lopez, mwenye umri wa miaka 24, 'anapiga ramli' kama asaini mkataba mpya na Atletico Madrid au la, zikiwa wiki tatu tangu ahusishwe na mpango wa kuhamia Tottenham na Arsenal.
Kiungo wa Tottenham, Jermaine Jenas, mwenye umri wa miaka 29, anaonekana kujiandaa kutua kwa mkopo Leeds, baada ya kuambiwa hayuko kwenye mipango ya Kocha Andre Villas-Boas.
TERRY NJE HADI CHELSEA NA QPR
Maumivu ya kifundo cha mguu ambayo yatakayomuweka nje beki John Terry, mwenye umri wa miaka 31, katika kikosi cha England, kitakachocheza mechi ya kuwania kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Ukraine kesho, yanatarajiwa kumuweka pia nje ya kikosi cha kikosi cha Chelsea kitakachocheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Queens Park Rangers Jumamosi.
Kocha wa Ukraine, Oleg Blokhin anataka kulipa kisasi dhidi ya England kesho katika kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia Uwanja wa Wembley kesho, kufuatia matokeo ya Euro 2012 baina ya timu hizo.
Kiungo wa England na Manchester City, James Milner, mwenye umri wa miaka 26, ameelezea siri ya mafanikio.
Beki wa kati wa Aston Villa, Ciaran Clark, mwenye umri wa miaka 22, amesema hawezi kuelewa uamuzi wa Giovanni Trapattoni kumuacha nje ya kikosi cha Jamhuri ya Ireland.
ALVES AWATULIZA MASHABIKI BRAZIL
Beki Dani Alves, mwenye umri wa miaka 29, amewataka mashabiki wa Brazil kutulia juu ya timu yao ya taifa, akiwaambia ni bora kukiunga mkono kikosi chao kichanga kuliko kuwazomea.


.png)
0 comments:
Post a Comment