![]() |
| Samatta kulia, hapa ilikuwa katika mechi na Zamalek. Leo ataiongoza tena Mazembe dhidi ya Berekum Chelsea nchini Ghana, je ataendelea kufunga mabao? |
Na Mahmoud Zubeiry
HATUA ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inatarajiwa kukamilika leo kwa mechi nne za
makundi yote, A na B kupigwa kwenye viwanja vine tofauti, kutafuta timu nne za
kuingia Nusu Fainali.
Katika Kundi
A, ASO Chlef watakuwa wenyeji wa Esperance ya Tunisia na Sunshine Stars
wataikaribisha Etoile du Sahel ya Tunisia pia, wakati Kundi B, Berekum Chelsea
ya Ghana itakuwa mwenyeji wa TP Mazembe
ya DRC, yenye washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas
Ulimwengu na wapinzani wa jadi wa soka ya Misri, Al Ahly na Zamalek watamenyana
mjini Cairo.
Mechi zote
za kukamilisha hatua hiyo, zitachezwa Saa 12:00 jioni zikianza na kumalizika
muda mmoja ili kukwepa kupanga matokeo.
Katika Kundi
A, Esperance inaongoza kwa pointi zake 13, baada ya kucheza mechi tano,
ikifuatiwa na Sunshine Stars yenye pointi saba, wakati ES Sahel ina pointi tano
katika nafasi ya tatu na ASO Chlef haina pa kwenda ikiwa mkiani na haina pointi
hata moja.
Kundi B ndio
kuna kazi, TP Mazembe na Al Ahly tayari zote zimevuna pointi 10 kila moja
ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine katika kundi lao, maana yake
zimekwishafuzu Nusu Fainali, tofauti na Kundi A, ambako Sunshine Stars na ES
Sahel zinawania kuungana na Esperance ambayo haing’oleki tena kileleni.
Lakini pia
Kundi B, Ahly na Mazembe inayoongoza kwa wastani wa bao moja zaidi, zote
zitapigania ushindi mnono ili kukwepa nafasi ya pili zisikutane na Esperance ya
Tunisia katika Nusu Fainali, kwani nayo inatisha. Zote zinaamini bora kukutana
na Esperance Fainali.
Lakini hata
timu ambazo hazina nafasi hazitalegea, kwa sababu zinapofanya vizuri
zinajiongezea bonasi kutoka kwenye mashindano, hivyo mechi zote zinatarajiwa
kuwa ngumu leo kwa sababu hata sare, au kila bao ni fedha.
MSIMAMO WA MAKUNDI:
KUNDI A
P W D L GF GA GD Pts
1 Esperance 5 4 1 0 7 2 5 13
2 Sunshine Stars 5 2 1 2 4 4 0 7
3 ES Sahel 4 1 2 1 1 1 0 5
4 ASO Chlef 4 0 0 4 3 8 -5 0
KUNDI B
P W D L GF GA GD Pts
1 TP Mazembe 5 3 1 1 9 5 4 10
2 Al Ahly 5 3 1 1 8 5 3 10
3 Berekum Chelsea 5 1 3 1 8 10 -2 6
4 Zamalek 5 0 1 4 4 9 -5 1
RATIBA NA MUDA WA MECHI ZA LEO:
ASO Chlef v Esperance (Saa 12:00
jioni)
Sunshine
Stars v ES Sahel (Saa 12:00 jioni)
Berekum
Chelsea v TP Mazembe (Saa
12:00 jioni)
Al Ahly v Zamalek (Saa 12:00 jioni)



.png)
0 comments:
Post a Comment