![]() |
| Nahodha Juma Kaseja akiwa ameinua Ngao akishangilia na wachezaji wenzake juzi |
Na Prince Akbar
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro
Premium Lager ambayo ni mdhamini wa vilabu vya Simba na Yanga, imeipongeza
Simba kwa kutwaa Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo na kusema ni ishara nzuri
ya matokeo mengine mazuri katika ligi kuu inayotarajiwa kutimua kivumbi
Jumamosi hii.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, alisema, “Tumefurahishwa sana kwa
ushindi huu wa Simba kwani ni ishara kuwa wamepania kutetea ubingwa wao vilivyo
msimu huu.”
Alisema mchezo wa Simba dhidi ya Azam ulikuwa mkali na wenye
ushindani mkubwa lakini Simba ilionyesha uwezo mkubwa na kweza kuibuka na
ushindi wa mabao 3-2.
“Siku zote sisi kilimanjaro Premium Lager tunajihusisha na
ushindi na ndio maana tumepania kuifikisha Soka ya Tanzania katika kilele cha
mafanikio,” alisema Bw Kavishe na kuongeza kuwa nia yao kama wadhamini ni
kuendelea kuona timu hizi zinafanya vizuri katika ligi kuu na mashindano
mengine yakiwemo ya kimataifa.
Katika taarifa yake Meneja huo alitoa rai kwa timu ya Yanga
pia kuhakikisha iaanza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Prisons
vizuri huko Mbeya wakati Simba itamenyana na African Lyon Jijini Dar es Salaam.
“Tunatumai kuwa timu hizi, zinazodhaminiwa na Bia yetu ya
Kilimanjaro Premium Lager, zitaonyesha nidhamu ya hali ya juu wakati wa ligi
hii na kuleta ushindani mkubwa kama ilivyo miaka yote,” alisema Kavishe.
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kukabidhi mabasi ya kisasa kwa timu hizi mbili hivi
karibuni.



.png)
0 comments:
Post a Comment