• HABARI MPYA

    Tuesday, January 08, 2013

    JERRY SANTO ASEMA BAHATI HAIKUWA YAO COASTAL UNION

    Santo katika mechi dhidi ya Azam Kombe la Mapinduzi

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    NAHODHA wa Coastal Union ya Tanga katika Kombe la Mapinduzi, Mkenya Jerry Santo amesema kwamba kutolewa kwao mapema katika michuano hiyo ya mwaka huu, kumetokana na kukosa bahati, lakini kama soka walicheza.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana usiku, Santo aliyewahi kuchezea Simba SC, alisema kwamba Coastal ilicheza soka nzuri na ndiyo maana haikufungwa hata mechi moja, lakini kwa kukosa bahati imetolewa.
    “Tulicheza vizuri, mechi zote tulipata nafasi lakini tulitumia moja tu, bahati haikuwa yetu, lakini timu yetu ni nzuri na tunaamini katika Ligi Kuu (ya Bara) tutafanya vizuri,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Tusker FC ya Kenya.
    Coastal Union ya Tanga ilitolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya sare ya bila kufungana na Miembani FC jioni ya jana kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung, Zanzibar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: JERRY SANTO ASEMA BAHATI HAIKUWA YAO COASTAL UNION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top